1 Corinthians 15:1-4

Kufufuka Kwa Al-Masihi

1 aBasi ndugu zangu nataka niwakumbushe kuhusu Injili niliyowahubiria, mkaipokea na ambayo katika hiyo mmesimama. 2 bKwa Injili hii mnaokolewa mkishikilia kwa uthabiti neno nililowahubiria ninyi. La sivyo, mmeamini katika ubatili.

3 cKwa maana yale niliyopokea ndiyo niliyowapa ninyi, kama yenye umuhimu wa kwanza: Kwamba Al-Masihi alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yasemavyo Maandiko, 4 dya kuwa alizikwa na alifufuliwa siku ya tatu, kama yasemavyo Maandiko,
Copyright information for SwhKC